Sport
Dollar
40,1901
0.22 %Euro
47,1146
0.08 %Gram Gold
4.336,9600
1.24 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Taifa hilo la Kusini mwa Afrika ni miongoni mwa nchi 36 ambazo utawala wa Trump unapanga kuongeza marufuku ya kusafiri
Zambia imewashauri raia wake wanaoishi ughaibuni, hasa Marekani, wasio na hadhi halali ya uhamiaji kufikiria kurejea nchini mwao kwa hiari, huku utawala wa Trump ukiweka uzito wa kupiga marufuku raia wa nchi 36 za ziada kuingia nchini humo.
Mwezi uliopita, Rais wa Marekani Donald Trump alitia saini tangazo la kupiga marufuku kuingia kwa raia kutoka nchi 12, hatua ambayo alisema inahitajika kulinda nchi yake dhidi ya "magaidi wa kigeni" na vitisho vingine vya usalama wa taifa.
Wakati huo huo, kebo ya ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje ilifichua fikira ya kupanua kwa kiasi kikubwa vikwazo vya usafiri kwa uwezekano wa kupiga marufuku raia kutoka nchi 36 za ziada, ikiwa ni pamoja na Zambia.
Maagizo hayo yalikuwa sehemu ya msako mkali wa uhamiaji ulioanzishwa na Trump mwanzoni mwa muhula wake wa pili mwezi Januari, ambao unajumuisha kuwafukuza wahamiaji wote wasio na vibali pamoja na kuwanyima kuandikishwa kwa baadhi ya wanafunzi wa kigeni.
'Kurudi kwa heshima'
"Marekani imetangaza hatua kadhaa muhimu za kuimarisha ulinzi wa mipaka yake na kwamba sheria na kanuni zake za uhamiaji zinafuatwa ipasavyo na raia wote wa kigeni," Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Zambia ilisema katika taarifa ya ushauri, ikiwataka raia walio nje ya nchi kufuata sheria na kanuni zote, kuzingatia kikamilifu sheria za uhamiaji, kuzingatia hali halali ya uhamiaji na uwezekani wa kujiondoa kwa hiari.
"Tunawahimiza Wazambia ... wasio na hadhi halali ya uhamiaji kufikiria kwa dhati kurejea Zambia kwa hiari, ili kuhakikisha wanarejea nyumbani kwa heshima," ilisema taarifa hiyo.
Hapo awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Mulambo Haimbe alisema nchi yake imepiga hatua katika kushughulikia maswala kadhaa ya serikali ya Marekani wakati inataka kukwepa kuwekwa kwenye orodha iliyopanuliwa ya marufuku ya kusafiri.
Comments
No comments Yet
Comment