Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Watekaji nyara wamewateka wanawake na watoto 10 katika tukio jipya la utekaji nyara nchini Nigeria, polisi wamesema siku ya Jumanne.
Tukio hili linafanyika huku wazazi wa watoto wengi waliotekwa kutoka shule ya Kikatoliki wiki iliyopita wakiwa na maombi ya kurejeshwa kwa watoto wao.
Polisi walisema shambulio lililotokea usiku wa Jumatatu katika jimbo la magharibi mwa Kwara lillenga kijiji cha Isapa, kijiji ambacho ni jirani na kijiji kilichoshuhudia kutekwa kwa angalau watu 35 wiki moja kabla.
Wiki iliyopita, kundi lenye silaha liliwateka watoto zaidi ya 300 kutoka shule ya Kikatoliki katika jimbo la Niger, kaskazini-kati mwa Nigeria; pamoja na wasichana 25 kutoka shule nyingine katika jimbo la Kebbi, kaskazini-magharibi, na wasichana 13 katika jimbo la Borno, mashariki mwa nchi hiyo.
Nigeria inakabiliwa na mgogoro wa usalama wa muda mrefu unaochochewa na mashambulio ya kigaidi na ukatili unaofanywa na “majambazi” wanaoshambulia vijiji, kuwaua watu na kuwateka nyara huku wakiitisha fidia.
Uchunguzi umeanza
Kamishna wa polisi wa jimbo la Kwara, Ojo Adekimi, alisema watekaji nyara katika shambulio hili jipya walikuwa wafugaji waliokuwa “wakifyatua risasi na kuwapora wanawake na watoto kutoka familia za wakulima wa eneo hilo.”
“Shughuli za kuwatafuta zimeanza. Polisi wako porini pamoja na wachunguzi wa kijiji,” aliliambia shirika la habari la AFP.
Aidha, kamishna huyo alisema mwanamke mmoja aliweza kutoroka na kurudi kijijini.
Shambulio hili limejiri wiki moja tu baada ya watekaji nyara kuwaua watu wawili na kuwateka nyara angalau waumini 35 katika shambulio la kanisani huko Eruku, takriban kilomita 20 kutoka Isapa. Waumini waliotekwa nyara tayari wamerejea nyumbani.
Comments
No comments Yet
Comment