Miongoni mwa wagombea waliokabidhiwa fomu zao za kugombea urais na makamu wa rais, ni George Gabriel Bussungu kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA).

Wagombea zaidi wa Urais Tanzania wapokea fomu zao za uteuzi kutoka kwa Tume huru ya Uchaguzi

Vyama mbalimbali vya kisiasa nchini Tanzania vinaendelea kuchukua fomu za wagombea wa kiti cha urais pamoja na makamu wake.

Miongoni mwa wagombea urais waliokabidhiwa fomu na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania za kugombea kiti cha urais na makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 11, 2025, ni George Gabriel Bussungu kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA).

Bussugu aliambatana na mgombea wake mwenza, Ali Makame Issa.

Kwa mujibu wa kalenda ya INEC, dirisha la kuchukua fomu hizo kwa nafasi ya uraia litakamilika Agosti 27.

#