Sport
Dollar
40,7413
0.03 %Euro
47,8361
0.51 %Gram Gold
4.404,8300
0.46 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Ikumbukwe kwamba, chama kikuu cha upinzani nchini humo, CHADEMA hakitoshiriki uchaguzi wa Oktoba 2025 baada ya kushindwa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, wakitaka kufanyike kwa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi nchini humo.
Idadi ya vyama vya siasa vilivyochukua fomu za kugombea nafasi ya Urais na Makamu wa Rais katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, utakaofanyika Oktoba 29, 2025, imefikia 11.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), jumla ya vyama vya siasa 14 vinatarajiwa kuchukua fomu hizo, zoezi lililoanza Agosti 9, 2025.
Hata hivyo, hadi kufikia Agosti 12, jumla ya vyama vya siasa 11 vilikuwa vimechukua fomu za kuwania nafasi ya Urais na Makamu wa Rais, katika uchaguzi wa Oktoba 2025.
Vyama hivyo ni pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Chama Cha Kijamii (CCK), Chama cha MAKINI, United Peoples’ Democratic Party (UPDP) na National League for Democracy.

Vingine ni National Reconstruction Alliance(NRA), Tanzania Labor Party (TLP), Union for Multiparty Democracy (UMD), Tanzania Democratic Alliance (TADEA) na Alliance for African Farmers Party (AAFP).
Comments
No comments Yet
Comment