OPEC+ imeongeza uzalishaji wa mafuta licha ya UAE kuamua kujiondoa katika muungano huo.

Uzalishaji wa Mafuta Waongezwa na OPEC+ Huku UAE Ikijitoa.

OPECt imeamua kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mafuta kwa mwezi Juni ili kukabiliana na mahitaji ya soko la kimataifa.

Hatua hiyo imekuja wakati United Arab Emirates imetangaza rasmi kujiondoa katika muungano huo, jambo linaloweza kubadilisha mwenendo wa soko la mafuta duniani,Wataalamu wanasema kuwa ongezeko la uzalishaji linaweza kusaidia kupunguza bei ya mafuta, lakini pia linaweza kuathiri mapato ya baadhi ya nchi zinazotegemea sana mafuta,

Uamuzi wa UAE umeelezwa kuwa unatokana na maslahi ya kitaifa, huku nchi hiyo ikitaka kuwa na uhuru zaidi katika sera zake za uzalishaji wa nishati,Hatua hizi mbili kwa pamoja zinaendelea kuibua mjadala kuhusu mwelekeo wa sekta ya nishati duniani.

Chanzo:Newstimeshub 

#