Kikao hicho kinakuja katikati ya mashambulizi mapya ya Wahouthi dhidi ya Saudi Arabia, na kusababisha hofu ya kiusalama kikanda.
Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan, zimekubaliana kuupa nguvu mkataba wa kiulinzi wa Makkah, siku ya jumatatu.
Katika tukio hilo, Uturuki iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, Waziri wa Ulinzi Yasar Guler na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi, Jenerali Selcuk Bayraktaroglu.
Kikao hicho kinakuja katikati ya mashambulizi mapya ya Wahouthi dhidi ya Saudi Arabia, na kusababisha hofu ya kiusalama katika kanda.
Wakati wa kikao hicho, Fidan alisema kuwa, mataifa hayo matatu yalijadiliana hatua za kuunga mkono usalama wa Saudi Arabia, na kutafuta njia zingine za kutatua migogoro ya kikanda.
Umoja huo, ulianzishwa mwezi Agosti kwa utaratibu kwamba shambulio la kijeshi dhidi ya nchi moja kati ya hizo tatu litachukuliwa na kuchukuliwa hatua kama shambulio dhidi ya nchi zote tatu, kwa kuzingatia ibara ya 5 ya NATO.
Washirika wataka ulinzi shirikishi
Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, ilisema kuwa, nchi hizo tatu zilikubaliana kuongeza vikosi vya kijeshi nchini Saudi Arabia.
Kulingana na wizara hiyo, Nauman Mahmood atahudumu kama Katiby Mkuu wa Umoja huo, kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kwa pamoja, washirika hao walilaani mashambulizi dhidi ya miji mitakatifu ya Makkah na Madinah, wakikubaliana kukabiliana na mashambulizi hayo.

