Kongamano hilo linatarajiwa kuidhinisha azimio la Baku na kutoa taarifa kuhusu ushirikiano katika masuala ya usalama na afya kwenye maeneo ya kazi.

Uturuki, mataifa mengine waondoka wakati rais wa Israel akihutubia kongamano la usalama Baku

Wawakilishi wa nchi mbalimbali, ikiwemo Uturuki, waliondoka ukumbini wakati rais wa Israel alipoanza hotuba yake katika kongamano la bara la Asia kuhusu usalama mji mkuu wa Azerbaijan, Baku.

Wakati Isaac Herzog alipoanza hotuba yake mchana wa siku ya Alhamisi katika mkutano wa CICA, wawakilishi wa nchi zaidi ya 10, ikiwemo Uturuki, waliondoka kwenye ukumbi huo.

Ujumbe wa Uturuki, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, pamoja na wawakilishi wa nchi zingine 10, waliondoka kwenye ukumbi huo wakati rais wa Israel akiendelea na hotuba yake kwa kongamano la CICA mjini Baku, TRT World iliripoti.

Hali kama hii ilijitokeza mwezi Septemba katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York wakati wa hotuba ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Kongamano hilo la siku moja la Alhamisi, ambalo mwenyeji wake ni Azerbaijan ikiwa mwenyekiti wa sasa wa CICA, linaleta pamoja wawakilishi wa mataifa wanachama, watathmini, na wadau wa mashirika ya kimataifa.

Majadiliano yataangazia ushirikiano katika kanda, uunganishaji, masuala ya kidijitali, na maendeleo endelevu chini ya uwenyekiti wa Azerbaijan.

Kongamano hilo linatarajiwa kuidhinisha azimio la Baku na kutoa taarifa kuhusu ushirikiano katika masuala ya usalama na afya kwenye maeneo ya kazi, pamoja na kutangaza mchakato wa kuijumuisha Laos kama mwanachama mpya.

Fidan baadaye alisema kuwa mataifa wanachama wa CICA lazima yawe na msimamo madhubuti katika kutetea haki za Wapalestina, ambayo ni moja ya mwanachama wake, pamoja na kupinga vikali unyanyasaji na ukiukwaji unaoendelea kwa sasa.

Tangu Oktoba 2023, Wapalestina zaidi ya 74,000 wameuawa na wengine zaidi ya 175,000 wamejeruhiwa Gaza kutokana na mauaji ya halaiki ya Israel, huku karibu asilimia 90 ya miundombinu ya eneo hilo ikiwa imeharibiwa.

Tangu wakati huo, misako ya Israel na mashambulizi ya walowezi wa Kiisrael dhidi ya Wapalestina na mali zao pia imeendelea katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, ikiwemo Jerusalem Mashariki.

#