Benki Kuu yasema kupungua kwa fedha za kigeni kunaweza kushusha thamani ya sarafu ya Uganda.
Benki Kuu ya Uganda imeonya kuwa kupitishwa kwa sheria mpya ya kudhibiti fedha za kigeni kunaweza kuongeza mfumko wa bei nchini kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu ya taifa.
Gavana Michael Atingi-Ego amesema sheria hiyo itapunguza mapato ya fedha za kigeni yanayoingia nchini, hali ambayo inaweza kudhoofisha akiba ya taifa na kuathiri kiwango cha ubadilishaji wa fedha.
Kwa mujibu wa BoU, kushuka kwa akiba ya fedha za kigeni kunaweza kusababisha sarafu ya Uganda kuporomoka dhidi ya dola ya Marekani, jambo litakaloongeza gharama za bidhaa na huduma.
Onyo hilo limekuja wakati mjadala wa mswada huo ukiendelea bungeni.