Haya yanajiri huku kukiwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambao umeenea katika mataifa kadhaa ya Afrika.

Uganda yakanusha kuwa na maambukizi ya Ebola baada raia wa Nigeria kuonesha dalili

Uganda imekanusha kuwepo kwa maambukizi ya Ebola baada ya Nigeria kuripoti kuwa mwanamke aliyeambukizwa ugonjwa huo alikuwa amesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika taarifa siku ya Jumanne, Wizara ya Afya ya Uganda imesema mwanamke huyo alipitia Uganda mapema mwezi wa Oktoba bila dalili zozote alipowasili kutoka Nigeria.

“Kusafiri kupitia Uganda hakumaanishi kuwa maambukizi yametokea hapa,” wizara ilisema, ikiongeza kuwa uchunguzi kuhusu eneo husika unaendelea.

Uganda inasema Nigeria bado haijatoa taarifa kamili za kusafiri za mwanamke huyo na watu aliotangamana nao.

‘Hakuna maambukizi’

“Tungependa kuweka wazi, wakati wa kutoa taarifa hii, Uganda HAINA maambukizi yoyote ya Ebola,” taarifa hiyo ilisisitiza.

Wizara inasema itaimarisha taratibu za uchunguzi wa afya katika maeneo ya mipakani, huku ikitoa wito kwa umma kuwa makini, kunawa mikono na kutumia vimiminika.

Nigeria ilithibitisha maambukizi yake ya kwanza ya mlipuko wa sasa wa Ebola siku ya Jumanne, huku Waziri wa Afya Muhammad Ali Pate akisema mwanamke huyo aliwasili mjini Abuja kwa ndege ya kimataifa akitokea Uganda.

#