Marekani na washirika wake wataka kulinda usafirishaji wa mafuta.
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inaandaa kuunga mkono juhudi zinazoongozwa na Marekani za kufungua tena Mlango Bahari wa Hormuz kwa kutumia nguvu.
Kwa mujibu wa ripoti, UAE inasukuma azimio katika Umoja wa Mataifa litakaloruhusu hatua za kijeshi kulinda njia hiyo muhimu ya mafuta.
Hatua hiyo inajiri wakati mvutano kati ya Iran na muungano wa Marekani na Israel unaendelea kuongezeka, huku Tehran ikitoa onyo kwa meli zinazopita bila uratibu.
Takribani asilimia 20 ya mafuta duniani hupitia katika mlango huo, hivyo hatua yoyote ya kijeshi inaweza kuwa na athari kubwa kiuchumi duniani.
CHANZO: Newstimehub