Waombaji watahitajika kuweka fedha kama dhamana kabla ya kusafiri Marekani
Marekani imepanua mpango wake wa dhamana za visa, ambapo sasa raia wa nchi 50 wanatakiwa kuweka hadi dola 15,000 kabla ya kupewa visa ya kuingia nchini humo. Lengo kuu ni kupunguza tatizo la watu kubaki Marekani baada ya muda wao wa visa kuisha.
Nchi 12 mpya zimeongezwa kwenye orodha hiyo, ikiwa ni pamoja na Ethiopia, Tunisia na Msumbiji. Maafisa wa serikali wanasema kuwa mpango huu umeonyesha mafanikio kwa kupunguza visa overstays, huku dhamana ikirejeshwa kwa wale wanaofuata sheria.
CHANZO: Newstimehub