Ongezeko la ndege linachangia huduma bora na biashara za kimataifa.
ATCL sasa inahudumia miji kadhaa ya Tanzania ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mtwara, Kigoma, Iringa, Pemba, Unguja, Songea, Mpanda, Tabora na Bukoba.
Pia, shirika lina mpango wa kuanza safari katika miji ya Sumbawanga, Musoma na Shinyanga. Kimataifa, ATCL inafanya safari za ndege kwenda Nairobi, Entebbe, Bujumbura, Lubumbashi, Lusaka, Harare, Johannesburg, Guangzhou (China), Mumbai (India) na Dubai. Huduma za usafirishaji mizigo pia zinachangia kukuza biashara na uchumi wa taifa.
CHANZO: Newstimehub