Kulingana na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi la Tanzania, David Misime, jumla ya silaha haramu 230 zimesalimishwa kwa hiyari, kufuatia kampeni ya kitaifa iliyozinduliwa Septemba 1, 2026.
Jumla ya bunduki 230 zimesalimishwa kwa hiyari nchini Tanzania, tangu tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa nchi hiyo, Patrobas Katambi, alipotangaza msamaha kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na kuwataka wazisalimishe kwa mamlaka husika.
Hatua hiyo inalenga kuwapa nafasi watu wenye silaha hizo kuzisalimisha kwa hiyari, kufuatia tangazo la msamaha lililotolewa na waziri huyo.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi la Tanzania, David Misime, jumla ya silaha haramu 230 zimesalimishwa kwa hiyari, kufuatia kampeni ya kitaifa iliyozinduliwa Septemba 1, 2026 na Katambi.
Kati ya silaha zilizosalimishwa ni pamoja na AK-47, Rifle, Shotgun, Mk IV 02, bastola na magobole.
Kifungu cha 62 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi, Sura ya 223, marejeo ya mwaka 2023, kinatoa adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, au faini ya Dola 5600 (Shilingi Milioni 15 za Kitanzania), au vyote kwa pamoja, kwa mtuhumiwa atakayekutwa na silaha kinyume cha sheria na kutiwa hatiani na mahakama kwa kosa la kupatikana na silaha haramu.
