Ethiopian Airlines yasema gharama za mafuta zimeongezeka kwa kasi.
Shirika la ndege la Ethiopian Airlines limetahadharisha kuwa linaweza kupandisha nauli za safari kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta kufuatia mgogoro wa Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa maafisa wa shirika hilo, bei ya mafuta imeongezeka kwa kiwango kikubwa ndani ya muda mfupi, hali inayosababisha changamoto katika kupanga safari na gharama za uendeshaji.
Aidha, baadhi ya safari kuelekea maeneo ya Mashariki ya Kati zimesitishwa, huku chache zikiendelea kama kawaida.
CHANZO: Newstimehub