Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Brigedia huyo wa jeshi ndiye afisa wa ngazi ya juu kuuawa katika vita hivyo vya muda mrefu tangu 2021.

Rais wa Nigeria athibitisha kuuawa kwa jenerali wa jeshi

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amethibitisha siku ya Jumanne kuwa magaidi walimuua brigedia jenerali wa jeshi, afisa wa ngazi ya juu kufariki katika vita hivyo vya muda mrefu tangu 2021.

ISWAP ilidai siku ya Jumatatu kuwa ilimvamia na kumuua kamanda mmoja eneo la Chad kaskazini, wakionyesha picha ya Brigedia Jenerali Musa Uba.

"Nimeskitishwa na kifo hiki cha wanajeshi na maafisa wetu waliokuwa kwenye mapambano. Mungu awafariji familia za Brigedia Jenerali Musa Uba na mashujaa wengine," Tinubu alisema katika taarifa.

Kwanza jeshi la Nigeria lilipinga taarifa hizo kuwa Uba alikamatwa waliposhambuliwa.

Kulingana na taarifa ya jeshi na Umoja wa Mataifa, wanajeshi wawili na sungusungu wawili waliuawa katika shambulio hilo.

ISWAP ilijitenga na kundi la kigaidi la Boko Haram 2016 na limejielekeza katika kushambulia jeshi la Nigerian.

Mashambulizi ya kigaidi yamewaua watu zaidi ya 40,000 na kufanya watu karibu milioni mbili kaskazini mashariki mwa kuondolewa katika makazi yao tangu 2009, na yameendelea hadi katika nchi jirani ya Niger, Chad na Cameroon.

Uba ni afisa wa pili mwandamizi wa jeshi kuuawa na magaidi katika kipindi cha miaka minne, baada ya Jenerali Dzarma Zirkusu, aliyeuawa Novemba 2021.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#