Dollar

43,0386

0.02 %

Euro

50,3281

-0.02 %

Gram Gold

6.171,2600

-0.74 %

Quarter Gold

10.399,3200

0.08 %

Silver

108,5400

-3.5 %

Mataifa ya Afrika yametoa wito wa kuheshimiwa kwa sheria ya kimataifa kufuatia kutekwa kwa Rais Nicolas Maduro, Cilia Flores na Marekani

Nchi za Afrika zaunga mkono Venezuela baada ya operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyomlenga Maduro
  • Umoja wa Afrika, unatoa wito wa majadiliano, kujizuia, na kulindwa kwa uhuru wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa, kwenye mazungumzo ya pamoja

    Nchi za Afrika zimeeleza kuunga mkono Venezuela kufuatia kutekwa kwa Rais Nicolas Maduro na Marekani, kusisitiza dhamira yao ya kuheshimiwa kwa sheria ya kimataifa.

    Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza siku ya Jumamosi kuhusu operesheni ya kijeshi Venezuela iliyosababisha Maduro na mkewe Cilia Flores kutekwa, na kuahidi kuweka utawala unaosimamiwa na Marekani kwa sasa, ikiwezekana na vikosi vya Marekani viwepo.

    Operesheni ya Marekani imefanya nchi za Afrika kutaka sheria ya kimataifa iheshimiwe na kueleza kuunga mkono taifa hilo la Marekani ya Kusini.

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa “moja kwa moja” amekataa hatua hiyo ya Marekani, ambayo “inadunisha uhuru wa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.”

    Siku ya Jumanne alitaka Maduro na mkewe waachiliwe, akisisitiza wito wa Afrika Kusini kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua “hatua madhubuti” ili isimamie jukumu lake na kuimarisha amani na usalama.

  • Afrika inadhihirisha wasiwasi wake kuhusu Venezuela katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

    Afrika Kusini imeliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kuwa mashambulizi “ya peke yao” ya Marekani nchini Venezuela na “kutekwa” kwa Maduro na mkewe “bila sababu ya msingi” ni ukiukwaji wa uhuru wa nchi hiyo na mipaka yake.

    Inasema hatua hizo “ni kinyume na taratibu zilizopo.”

    “Kwa mara nyingine tena, imani kuwa mwenye nguvu ndiye mwenye haki, inajidhihirisha na diplomasia inadunishwa,” ilisema.

    Afrika Kusini inasema historia inajirudia kuwa “uvamizi wa kijeshi” wa mataifa huru unasababisha ukosefu wa usalama na matatizo makubwa zaidi, wakieleza mfano wa Libya, Iraq na baadhi ya nchi za Afrika, ambapo wanasema kuingilia kwa mataifa ya nje kumesababisha ukosefu wa usalama kudunisha taasisi za kitaifa za utawala.

    Umoja wa Afrika, mataifa yaeleza wasiwasi wao kwa hatua ya Marekani

    Umoja wa Afrika (AU) ilieleza kuhusu “kutekwa kwa” Maduro na uvamizi wa Venezuela, ukisisitiza dhamira kwa sheria ya kimataifa.

    “Changamoto za ndani zinazokabili Venezuela zinaweza kutatuliwa kwa mjadala wa kisiasa unaojumuisha watu wa Venezuela wenyewe,” ulisema katika taarifa.

    Ulitaka pande zote kujizuia na kuhakikisha kuwa kuna amani na usalama katika kanda, huku wakiunga mkono watu wa Venezuela.

    Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) pia ilisisitiza heshima kwa uhuru wa Venezuela na mipaka yao, ukieleza pamoja na kuwa mataifa yana haki ya kupambana uhalifu wa kimataifa, hatua kama hizo lazima ziwe kulinga na sheria ya kimataifa.

    Ghana ilishtumu kile walichokiita “uvamizi usio wa msingi” wa Venezuela na “utekaji” wa Maduro na mkewe, wakitaka waachiliwe na kusitisha vurugu mara moja.

    Mawaziri wa mambo ya nje wakiunga mkono uhuru wa nchi katika mazungumzo na mwenzao wa Venezuela

    Katika mazungumzo kadhaa kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Yvan Gil, mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika walieleza kuwaunga mkono watu wa Venezuela, kuthibitisha dhamira yao ya kuheshimu sheria ya kimataifa na uhuru.

    Waziri wa Senegal Cheikh Niang alieleza kuwa watu wa Venezuela wana haki ya kujitawala wenyewe.

    Karamoko Jean Marie Traore wa Burkina Faso alishtumu operesheni hiyi kama ukiukwaji wa utaratibu wa Umoja wa Mataifa.

    Abdoulaye Diop wa Mali alishtumu mashambulizi kwa raia na maeneo ya kijeshi, na Mbae Mohamed wa Visiwa vya Comoro akieleza kuhusu “mashambulizi ya mabomu yasiyo na msingi na utekaji nyara” wa Maduro na mkewe.

    Abdoulaye Sabre Fadoul wa Chad alisisitiza kuheshimiwa kwa Utaratibu wa Umoja wa Mataifa, Tete Antonio wa Angola akashtumu uvamizi “wa mataifa ya kigeni,” na Yaou Sangare Bakary wa Niger amesema operesheni hiyo inatishia mataifa yote yanayoendelea.​​​​​​​

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#