Dollar

42,7376

0.04 %

Euro

50,2245

0.06 %

Gram Gold

5.953,2400

-0.17 %

Quarter Gold

9.828,8400

0.04 %

Silver

89,8300

-1.63 %

Kuwa mwenyeji wa mashindano kunawapa Morocco hamasa na nafasi nzuri, lakini pia kunaibua kumbukumbu za kushindwa kufanikiwa hapo awali na wamekuwa na hamu ya muda mrefu ya kupata ushindi.

Morocco ina jukumu kubwa wakati ikibeba matarajio ya uwenyeji AFCON 2025

Wenyeji wa mashindano ya Mataifa ya Afrika Morocco wamejipanga vilivyo wakiwa na viwanja vya kutosha na vya kupendeza kwa ajili ya timu zote 24.

Timu hiyo inayoorodheshwa kama bora zaidi barani Afrika ilifika hatua ya nusu fainali kwenye michezo ya Kombe la Dunia iliopita, wameshinda mechi 18 mfululizo na wana kikosi cha wachezaji mahiri wanaokipiga katika vilabu vikubwa vya Ulaya, kuwafanya kutajwa miongoni mwa wanaotarajiwa kuchukuwa ubingwa.

Lakini licha ya nafasi yao muhimu katika mechi za Afrika, Morocco imeshinda kombe hilo mara moja tu, na hiyo ilikuwa karibu nusu karne iliopita. Walipewa nafasi kubwa katika mashindano makala manne yaliyopita lakini walishindwa kupenya zaidi ya robo fainali.

Kucheza nyumbani kunawapa nafasi kubwa na kumekuwa na juhudi kubwa za maandalizi.

“Lazima tushinde AFCON,” alisema kocha Walid Regragui katika mkutano wa mwisho na waandishi wa habari mwezi uliopita.

"Nyumbani, tutajitahidi zaidi; tumeonesha tunaweza.

Tumeimarika sasa,” alisema kuhusu kuondolewa katika hatua ya 16 bora na Afrika Kusini miaka miwili iliopita.

Viwanja vinavyovutia

Morocco watakuwa wenyeji mwenza wa Kombe la Dunia 2030 pamoja na Ureno na Uhispania na AFCON inafaidi kwa kutumia viwanja tisa katika miji sita, ikiwa ni ya kwanza kwa mashindano hayo ya Afrika.

Mechi tatu za kwanza Morocco katika uwanja uliokarabatiwa wa Stade Prince Moulay Abdellah mjini Rabat, wenye uwezo wa kuingia mashabiki 68,700, ambapo mechi ya ufunguzi na fainali zitachezwa.

Kuna uwanja mwingine mjini Tangier wenye uwezo wa mashabiki 75,000 pia utatumika kwa mechi za nusu fainali, pamoja na Agadir, Casablanca, Fes na Marrakech.

Mabingwa watetezi Ivory Coast, Nigeria na Senegal wanaongoza azimio la Afrika Magharibi, huku Afrika kaskazini ikiwa na Algeria na Misri ambao wanatarajiwa kugombea vilivyo ubingwa.

Hakun timu ngeni kwenye mashindano haya, ingawa wote Botswana na Visiwa vya Comoro wanacheza michuano hii kwa mara ya pili.

Comoro wanafahamika kama wanaoangusha mibuyu katika mechi za 2021 walipowafunga Ghana nchini Cameroon na safari hii wanacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya wenyeji Morocco siku ya Jumapili.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#