Masemola alishtumiwa kukiuka sheria za manunuzi katika zabuni ya polisi ya 2024 ambayo tayari imesitishwa.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anasema mkuu wa polisi nchini humo aliyekuwa amesimamishwa kazi anaweza kurudi kazini baada ya waendesha mashtaka kumuondolea kesi ya ufisadi dhidi yake, ofisi ya rais ilisema siku ya Ijumaa.
Ramaphosa alimsimamisha kazi Kamishna wa Polisi Fannie Masemola mwezi Aprili baada ya mkuu huyo kuhusishwa na sakata la zabuni ya huduma ya afya la Dola milioni 20.
Masemola alishtumiwa kwa kukiuka sheria za manunuzi 2024 katika zabuni ambayo kwa sasa imesitishwa ya polisi kupata huduma ya afya iliyokuwa imepewa mfanyabiashara Vusimuzi "Cat" Matlala, ambaye anadaiwa kuhusika na magenge ya uhalifu.
Lakini mahakama ya mji mkuu Pretoria ikamuondolea lawama Masemola mwezi uliopita baada ya waendesha mashtaka kupendekeza kuondoa kesi dhidi yake.
Ramaphosa anasema mkuu huyo wa polisi "ruhsa kurudi kwenye majukumu yake" siku ya Jumatatu, ofisi ya rais ilisema.
Mwezi Julai 2025, Ramaphosa aliteua tume ya kuchunguza ufisadi kwenye mfumo wa haki wa nchi hiyo.
Vikao vya tume hiyo vilifuatiliwa na watu wengi, na kusababisha kusimamishwa kazi kwa waziri wa masuala ya polisi Senzo Mchunu na zaidi ya maafisa wengine 10 waandamizi.
Tume hiyo inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake mwezi Januari.

