Iran imesema Marekani imejibu pendekezo lake la amani huku mazungumzo yakiendelea kwa tahadhari.
Iran imetangaza kuwa imepokea majibu kutoka United States kufuatia pendekezo lake la hivi karibuni la kumaliza mgogoro.
Pendekezo hilo lililowasilishwa kupitia wapatanishi lililenga kupunguza mvutano katika eneo la Ghuba, ikiwa ni pamoja na kufungua njia za usafırishaji wa mafuta na kuondoa baadhi ya vikwazo vya kiuchumi,
Hata hivyo, Marekani imeonyesha kutoridhishwa na baadhi ya vipengele vya pendekezo hilo, hasa kutokuwepo kwa makubaliano ya wazi kuhusu udhibiti wa shughuli za nyuklia za Iran. Licha ya tofauti hizo, pande zote zinaendelea kuwasiliana, jambo linaloashiria uwepo wa juhudi za kidiplomasia za kutafuta suluhisho la kudumu,
Wachambuzi wanaona kuwa hatua hii ni muhimu katika kupunguza mvutano uliosababisha athari kubwa kwa uchumi wa dunia, hasa katika sekta ya nishati.
Chanzo:Newstimeshub