CENTCOM yatekeleza zuio kamili dhidi ya meli zinazoingia na kutoka Iran baada ya mazungumzo kushindikana.
Mvutano umeongezeka zaidi baada ya Marekani kupitia CENTCOM kutangaza kuwa imefanikiwa kusimamisha kabisa usafirishaji wa baharini kwenda na kutoka Iran.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo ilianza rasmi Jumatatu na inalenga meli zote bila kujali taifa zinapotoka au zinapokwenda, mradi tu zinahusiana na bandari za Iran.
Hatua hiyo ilitangazwa na Donald Trump, ambaye alisema kuwa ni matokeo ya kushindikana kwa mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Marekani na Iran.
Ndani ya saa 24 za kwanza, hakuna meli iliyofanikiwa kuvuka kizuizi hicho, huku baadhi ya meli zikilazimika kurejea bandari walikotoka.
Hatua hii imezidisha hofu ya kuongezeka kwa mzozo wa kijeshi katika eneo hilo nyeti la kimkakati.