Serikali ya Mali yatangaza operesheni maalum za kijeshi kufuatia mashambulizi katika miji kadhaa.
Serikali ya Mali imetangaza kuimarisha hatua za usalama na kuanzisha operesheni maalum za kijeshi baada ya mashambulizi ya hivi karibuni yaliyolaaniwa na Umoja wa Afrika.
Maafisa wa jeshi wamesema vikosi vya ziada vimetumwa katika mji mkuu Bamako pamoja na maeneo ya Gao, Kidal na Sevare ili kuzuia mashambulizi mengine yanayoweza kutokea.
Hatua hiyo inafuatia kauli ya Umoja wa Afrika kulaani mashambulizi hayo na kueleza wasiwasi kuhusu usalama wa raia.
Serikali ya Mali imesisitiza kuwa itaendelea kuwafuatilia wahusika wa mashambulizi hayo hadi wahakikishe kuwa usalama umerejeshwa kikamilifu katika maeneo yote yaliyoathirika.