Dollar

42,5113

-0.02 %

Euro

49,6449

-0.1 %

Gram Gold

5.736,9200

-0.28 %

Quarter Gold

9.512,2800

0 %

Silver

78,1200

0.08 %

Wataalamu wa afya wamepongeza hatua hiyo katika kudhibiti wimbi la maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Malawi yaidhinisha matumizi ya sindano ya dawa ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)

Malawi imeidhinisha matumizi ya sindano za kufubaza VVU ijulikanayo kama lenacapavir, na kuwa taifa la nne barani Afrika kupitisha dawa hiyo.

Dawa hiyo iliyotengenezwa na kiwanda cha Gilead Sciences Ireland, UC, hutolewa kupitia sindano, kila baada ya miezi sita.

Mamlaka ya Udhibiti Madawa na Famasia nchini Malawi (PMRA) ilipitisha dawa hiyo kufuatia siku 46 za majaribio.

Kulingana na Dkt. Beatrice Matanje, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Ukimwi nchini humo (NAC), amepongeza hatua hiyo, akiiita ni ya muhimu ya kupambana na VVU nchini humo.

“Uidhinishwaji huu ni hatua muhimu katika mapambano dhidi ya VVU. Tumehamasika na uamuzi huu wa kupunguza maambukizi ya VVU kwa raia wa Malawi,” alisema Matanje.

Mbali na Malawi, nchi zingine zilizoidhinisha dawa hiyo ni pamoja na Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe.

Uamuzi wa kuidhinisha dawa hiyo unakuja wakati Malawi inaendelea kupambana na wimbi la maambukizi, ambayo yanakadiriwa kuwa ya juu zaidi ulimwenguni.

Takriban watu 950,000 nchini Malawi, wengi wakiwa ni wanawake na watoto wanaishi na VVU, kulingana na Tume ya Ukimwi nchini humo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#