Kati ya maeneo ya afya 66 yaliyoathirika kufikia sasa, 50 yameripoti maambukizi yasiyopungua moja ambayo yamethibitishwa ndani ya siku 21, kulingana na ripoti.
Maambukizi ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yanaendelea kuenea huku zaidi ya robo tatu ya maeneo ya afya yakiathirika tangu kuanza kwa mlipuko huo mwezi Mei, Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika limesema katika ripoti yao ya tathmini siku ya Jumatano, huku maambukizi yakikaribia 10,000.
Ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo vimeathiri mikoa minane: Haut-Uele, Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Bas-Uele, Tshopo, Ubangi Kusini na Ubangi Kaskazini.
Idadi ya maambukizi ya Ebola yaliyothibitishwa Congo imepita 9,600, ikiwemo vifo 4,646 tangu mlipuko huo kutangazwa, kulingana na data za WHO.
Kati ya maeneo ya afya 66 yaliyoathirika kufikia sasa, 50, au asilimia 75.8, yameripoti maambukizi yasiyopungua moja ndani ya kipindi cha siku 21, ripoti hiyo ilionesha.
Maambukizi yaliyothibitishwa
Ituri inaendelea kuwa na maambukizi mengi zaidi ikiwa ni asilimia 72.7, kuhusu maambukizi ya kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ni kwa mikoa ya Kivu Kaskazini na Haut-Uele.
Katika wastani wa siku saba za hivi karibuni inaonesha maambukizi kuongezeka, ishara ya kuenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, ripoti hiyo ilisema.
WHO imesema mlipuko huo umekuwa hatari zaidi, ukihusishwa na maambukizi ya nchini Kenya na yale yaliyotambuliwa Nigeria.
Kenya imethibitisha maambukizi mengine ya Ebola siku ya Jumanne, na kufanya jumla ya maambukizi hayo kufikia tisa.
