Dollar

39,0359

0.28 %

Euro

44,0569

-0.05 %

Gram Gold

4.134,9200

0.28 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mcroatia huyo ameichezea Real Madrid jumla ya mechi 600 toka alipojiunga nao mwaka 2012, akitokea Tottenham ya Uingereza.

Luka Modric kuachana na Real Madrid baada ya fainali za Kombe la Dunia kwa upande wa klabu

Kiungo Mcroatia anayekipiga katika klabu ya Real Madrid, ametangaza kuachana na vigogo hao wa nchini Hispania mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu itakayofanyika kuanzia Juni 14 hadi Julai 13, 2025.

"Kila kitu maishani kina mwanzo na mwisho wake…jumamosi hii nitacheza mechi yangu ya mwisho kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu," alisema Modric, mwenye umri wa miaka 39, kupitia ukurasa wake wa Instagram.

"Ninaondoka nikiwa na furaha, fahari na kumbukumbu zisizosahaulika.

 "Licha ya kuwa sitoendelea kuvaa jezi hii baada ya Kombe la Dunia kwa upande wa Klabu, nitaendelea kuwa shabiki wa Real Madrid."

Mcroatia huyo ameichezea Real Madrid jumla ya mechi 600 toka alipojiunga nao mwaka 2012, akitokea Tottenham ya Uingereza.

Katika safari hiyo, Modric ameshinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara sita, kombe la Mfalme mara mbili, Ligi Kuu mara nne, kati ya mataji 28 aliyobeba ndani ya uzi mweupe wa ‘Los Blancos’.

Modric, ambaye alipewa jukumu la unahodha wa Real Madrid msimu uliopita, alitwaa tuzo ya Ballon d'Or mwaka 2018, kutokana na kipaji chake alichokionesha Real Madrid, na ndani ya jezi ya timu ya taifa ya Croatia, ambayo aliisaidia kufika hatua ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#