Rais wa Taiwan ametembelea Eswatini ili kuimarisha uhusiano wa kisiasa na maendeleo kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Taiwan, Lai Ching-te, ameanza ziara yake nchini Eswatini kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili,Ziara hiyo imejikita katika kujadili fursa za uwekezaji, miradi ya maendeleo, pamoja na ushirikiano katika sekta muhimu kama afya na elimu.
Katika mikutano yake na viongozi wa Eswatini, akiwemo Mfalme Mswati III, Rais Lai alisisitiza umuhimu wa urafiki wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili na kuahidi kuendelea kutoa msaadawa maendeleo,
Eswatini ni mshirika muhimu wa Taiwan barani Afrika, na imekuwa ikiiunga mkono katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa, licha ya shinikizo kutoka mataifa mengine.
Wachambuzi wanaeleza kuwa ziara hiyo inaonyesha dhamira ya Taiwan ya kuendeleza uhusiano wake na washirika wachache waliobaki, huku ikijaribu kupanua ushawishi wake kimataifa.
Kwa upande mwingine, Eswatini inanufaika na ushirikiano huo kupitia misaada ya kiuchumi na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Taiwan.
Chanzo:Newstimeshub