Mkataba huo, unafuatia ule wa Juni 2024, uliosainiwa kati ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini, kuhusu ushirikiano wa kijeshi, iwapo moja ya nchi hizo zitavamiwa.
Korea Kaskazini na Urusi, zimetiliana saini mkataba wa miaka mitatu, wa kushirikiana katika kukabiliana na majanga.
Mkataba huo, umesainiwa baada ya kikao cha mawaziri kutoka pande zote mbili, jijini Pyongyang.
Kulingana na Shirika la Habari la Korea (KCNA), Waziri wa Kukabiliana na Majanga wa Korea Kim Chol Nam, alifanya kikao na mwenzake wa Urusi, Alexandr Kurenkov, siku ya Jumatatu.
Wakati wa kikao hicho, pande hizo mbili zilibadilishana uzoefu na mafanikio, ya namna ya kukakibiliana na majanga na namna bora za kushirikiana katika jambo hilo.
Mkataba huo, unafuatia ule wa Juni 2024, uliosainiwa kati ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini, kuhusu ushirikiano wa kijeshi, iwapo moja ya nchi hizo zitavamiwa.