Mazoezi ya kijeshi ya Misri karibu na Israel yameibua tahadhari kuhusu usalama wa eneo hilo.

Jeshi la Misri Lafanya Mazoezi ya Risasi Halisi Mpaka wa Israel.

Egypt imefanya mazoezi ya kijeshi ya risasi halisi karibu na mpaka wake na Israel, hatua iliyovuta hisia za kimataifa,

Jeshi la Misri limesema kuwa mazoezi hayo ni ya kawaida na yanalenga kuimarisha utayari wa wanajeshi katika kulinda mipaka ya taifa.Wataalamu wa usalama wanasema kuwa mazoezi ya aina hii, hasa yanapofanyika karibu na mipaka, yanaweza kuibua tahadhari hata kama hayana lengo la uchokozi,

Hata hivyo, hakuna taarifa ya tukio lolote la kiusalama lililoripotiwa wakati wa mazoezi hayo, na hali inaendelea kuwa tulivu.

Hatua hiyo inaonyesha umuhimu wa nchi kuendelea kujiandaa kijeshi licha ya kuwepo kwa mikataba ya amani katika eneo hilo.

Chanzo:Newstimeshub 

#