Urithi wa viungo vya Zanzibar unatoa taswira ya biashara, utumwa na himaya. Leo hii, juhudi za kuendeleza urithi huo unaibua historia, kukumbusha vizazi kuhusu historia yao na kuwaunga mkono wakulima wa viungo wanawake.

NEWSTIMETR
NEWSTIMETR
Himaya, kumbukumbu, na kuhifadhi urithi wa viungo vya Zanzibar

Na Adama Juldeh Munu

Harufu ya karafuu, mdalasini inapitiza katika Makumbusho ya Viungo ya Zanzibar, kuadhimisha sifa yake ya muda mrefu ya ‘Kisiwa cha Viungo’, kutokana na nafasi yake kama kitovu cha biashara ya viungo duniani, hasa wakati wa karne za 18 na 19.

Lakini hii siyo tu hafla ya kusherehekea historia ya viungo inayonasibishwa na eneo hilo. Kuna umuhimu kwa historia ya utumwa, himaya, na njia za biashara zilizounganisha frika Mashariki na Mataifa ya Kiarabu, Asis Kusini, na Ulaya.

Ilizinduliwa na Wakfu wa Assalam Community Agosti 2025, inasemekana kuwa makumbusho ya kwanza ya aina hii barani Afrika, ikileta pamoja kumbukumbu ya yaliyojiri, simulizi na kujumuika.

Moja ya taswira ya kupendeza ni namna inavyokuonesha historia ya njia za biashara kwa video na viungo vilivyofikishwa kote duniani.

Wasanifu wataalamu wa eneo hilo walisaidia katika kuimarisha muonekano wa makumbusho hayo, ambayo yameundwa kwa bidhaa rejeshi kuonesha ishara ya rangi, usanifu na taswira za kisiwa hicho cha viungo.

Lakini makumbusho hiyo pia ni juhudi za kubadilisha namna jamii za eneo hilo - ikiwemo vijana - wanavyofahamu elimu ya kitamaduni na kihistoria, ambayo, kulingana na ripoti ya UNESCO, ni kwa uchache.

Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2022 inaonesha kuwa chini ya humusi ya mitaala ya Afrika Mashariki inajumuisha elimu ya urithi, kumaanisha vizazi vya sasa havina uelewa wa yaliyojiri zamani.

Wanasema tangu kuzinduliwa kwake, mamia ya wanafunzi kati ya miaka 9 na 19 wameshiriki katika warsha, na usanifu wa Kanga, ufinyanzi, utengenezaji sabuni na and traditional weaving.

“Lengo letu ni kueleza simulizi ya Zanzibar ambayo haijaelezwa - siyo tu kupitia uzuri na umuhimu wa viungo, lakini kupitia historia ya muda mrefu. Makumbusho haya pia yanaangazia kituo cha elimu - sehemu ambayo watoto na watu wazima wataweza kujifunza historia, sayansi, jiografia, ikolojia, na usanii kwa njia ya kujumuika. Kwa kuunganisha masuala ya kale na ya sasa, tunalenga kuhamasisha, uponaji, na fikra pevu kwa vizazi vijavyo”, makumbusho hayo yameelezea TRT Afrika.

Mtaa wa viungo

Makumbusho ya Njia ya Viungo iko katika mtaa wa kisiwa hicho wa Stone Town, Urithi wa Dunia wa UNESCO uliokuwepo tangu kale na ulio na vichochoro vyembamba, majengo ya kale na milango ya kipekee iliotengenezwa kwa mbao.

Biashara ya viungo ilishamiri kabla ya ukoloni, ikianza enzi za wafanyabiashara wa Kiarabu na Kifarsi karne ya 8, kama sehemu ya mtandao wa biashara ya Bahari Hindi.

Miongoni mwa viungo maarufu viliohusishwa na biashara hiyo ilikuwa ni karafuu, na mdalasini, pilipili manga, binzari, na vanilla.

Himaya ya Ureno ilikuwa watawala ya kwanza wa Ulaya kufika Stone Town karne ya 16. Ngome Kongwe, ndiyo jengo la kale zaidi eneo la Stone Town, lililojengwa na Waarabu wa Oman, Busaidi katika sehemu palipokuwa kanisa la Kireno mwaka 1698.

Kufikia karne ya 17, utawala wa Sultan wa Oman ukaanza kutawala Zanzibar, ambapo kukawa sehemu muhimu ya biashara ya bandari, hasa meno ya tembo, viungo na watumwa.

Viungo vilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Harufu nzuri ya vyakula vya Kiswahili inatokana na viungo hivyo, iwe ni pilau ya kuku ilioungwa kwa binzari na pilipili manga, biryani, au mahamri. .

Pia wanatumia kama tiba asilia. Chai ya karafuu inaweza kuondoa muwasho kooni, na tangawizi husaidia kuimarisha kinga ya mtu. Katika harusi, mafuta ya karafuu na liwa hutumiwa kama uturi kwa bibi harusi, huku udi uliotengenezwa kwa viungo unachomwa katika majumba na sehemu za ibada.

Uhusiano wa Zanzibar na viungo unadhihirisha uwezo wa urithi kijiografia, biashara na utamaduni. Huku historia ya biashara ya viungo ikipungua katika karne kadhaa zilizopita, umuhimu wake kwa jamii hizo bado uko pale pale, na wanajitahidi kuulinda.

TRT Afrika — TRT Afrika

#