Chanjo hizo zilichukuliwa kutoka eneo la Mradi wa Afya la Bandim, unaoongozwa na watafiti wa Denmark kuhusu majaribio ya homa ya ini.
Polisi nchini Guinea-Bissau wamekamata shehena ya chanjo kutoka kituo kinachohusishwa na majaribio ya chanjo ya homa ya ini kwa watoto wachanga ambayo WHO iliyataja kuwa "kinyume na maadili".
Utafiti huo, ulitakiwa kufanyika kwa watoto wachanga 14,000 katika taifa hilo maskini la Afrika ya magharibi na walitakiwa kupewa chanjo ya homa ya ini, lakini ulisitishwa hadi pale kutakapofanyika tathmini, WHO ilisema mwezi Februari.
Uchunguzi wa polisi wa mahakama wa Guinea-Bissau siku ya Jumatatu uliidhinisha msako "na kukamata shehena ya chanjo za homa ya ini zilizokuwa zitumike kwa watoto nchini humo".
Chanjo hizo zilipatikana kwenye Mradi wa Afya wa Bandim, unaoongozwa na watafiti wa Denmark katika majaribio ya chanjo ya homa ya ini.
Utafiti wa awali wa raia hao wa Denmark umeangalia madai ya hatari ya chanjo hiyo, na mfumo wao umemulikwa na wanasayansi.
‘Usalama wa chanjo’
Vituo vya Kudhibiti Ugonjwa vya Marekani vilikuwa vimetoa Dola milioni 1.6 kwa ajili ya majaribio ya Guinea-Bissau.
Guinea-Bissau ina tatizo kubwa la homa ya ini na "kuzuia utoaji wa chanjo kunaweza kuhatarisha maisha ya watoto zaidi, na hiyo kumaanisha hata vifo", Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema mwezi Februari.

