Kauli hii inakuja wakati ambapo Iran na Marekani zinaendelea na majadiliano Oman, huku Uturuki ikifanya mawasiliano na pande zote mbili ili kuzuia mgogoro wa kikanda.

Fidan wa Uturuki akataa mashambulizi ya anga kama njia ya kubadilisha uongozi wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema mashambulizi ya anga dhidi ya Iran hayataangusha serikali, huku akikataa madai kwamba hatua za kijeshi zinaweza kuleta mabadiliko ya uongozi.

"Hapana, haitaanguka," Fidan amesema katika mahojiano na CNN Turk siku ya Jumatatu alipoulizwa iwapo serikali ya Iran itaanguka kama itashumbuliwa.

"Sitaki kutabiri mazingira kadhaa nchini Iran, lakini utawala hauwezi kubadilika kupitia mashambulizi ya anga. Hiyo ni ndoto," amesema.

Fidan ameongeza kwamba, wakati hatua za kijeshi zinaweza kudhoofisha serikali, haiwezi kuleta mabadiliko ya serikali.

"Kinachotokea ni serikali kudhoofika, mfumo kudhoofika, na itashindwa kutoa huduma kwa watu. Halafu, serikali iliyopo inaweza kuamua kufanya maamuzi magumu na pengine kurekebisha hali. Inaweza kujibadilisha yenyewe," amesema.

Jitihada za kidiplomasia za Uturuki

Kauli yake imekuja wakati Iran na Marekani zikijiandaa kwa majadiliano mengine, ambayo yameanza Oman siku ya Ijumaa baada ya kusitishwa kwa takriban miezi nane.

Akisisitiza kwamba, wasi wasi kuhusu Iran umetawala agenda ya kimataifa, huku akitahadharisha kwamba, eneo hilo haliwezi kuhimili tena mgogoro mwengine.

"Rais wetu Recep Tayyip Erdogan pia anaonesha kuguswa na suala hili. Kwa hiyo, tunataka kutumia njia zote kuzuia uwezekano wa vita," amesema.

Fidan amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amemtaarifu kuhusu majadiliano yanayoendelea na kusema kuwa Uturuki pia imekuwa katika mawasiliano na Marekani.

Ameielezea hali hiyo kuwa ni "ngumu kupata utatuzi wa haraka," hata hivyo ameweka wazi utayari wa pambe zote kuendelea na mazungumzo.

Amesema kumekuwa na wito wa "kubuni suluhu zaidi" na kusisitiza haja ya kuachana na "vitisho vya vita."

"Kwa sasa, hakuna tishio la vita," Fidan amesema, na kuongeza kuwa mlango wa majadiliano umefunguliwa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#