Kulingana na Erdogan, Uturuki imepiga hatua kubwa, ndani ya muda mfupi, licha ya changamoto ilizokutana nazo, akisisitiza kuwa nchi hiyo itaendelea kuwekeza katika fursa zote, kuhakikisha lengo linatimia.
Rais Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa Uturuki itaendelea na mkakati wake wa anga za mbali, ili ijijengee heshima katika nyanja hiyo.
“Hatutoruhusu engo letu lisitimie, hadi tuhakikishe kuwa Uturuki inapata heshika katika eneo hili,” alisema Rais Erdogan wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 77 wa anga za mbali, uliofanyika Antalya.
Kulingana na Erdogan, Uturuki imepiga hatua kubwa, ndani ya muda mfupi, licha ya changamoto ilizokutana nazo, akisisitiza kuwa nchi hiyo itaendelea kuwekeza katika fursa zote, kuhakikisha lengo linatimia.
Katika hatua nyingine, Rais Erdogan aliweka wazi kituo cha uzalishaji kitakachokuwa chini kituo cha utafiti wa mambo ya mwezini.
Kituo hicho, chenye uzito wa tani 3.5, kina uwezo wa kuzalisha kwa asilimia 80, alisema Erdogan.
Erdogan alianisha miradi ya Türksat 6A, kama ushuhuda wa maendeleo katika sekta ya anga.
Kulingana na Erdogan, mradi huo utaboresha sekta na kufanikisha ufikiaji wake, na kutoa msaada kwa bara la Afrika.
Zaidi ya washiriki 10,000 na wawakilishi kutoka mataofa 100, wanashiriki katika kongamano hilo.
Wakati huo huo, Rais Erdogan amesisitiza kuwa, si vyema sekta ya anga ikadhibitiwa na nchi chache, akitadhaharisha kuhusu matumizi ya eneo hilo kwa mashindano ya kijeshi.
“Eneo la anga za juu sio la kugombania wala kuonesheana ubabe,” alisema.
Kongamano hilo la Antalya, linafanyika chini ya Kauli Mbiu isemayo “The World Needs More Space”, ikiwaleta pamoja wanasayansi, wahandisi, watunga sera na mashirika ya anga kujadili namna ya kukuza teknolojia na ushirikiano wa kimataifa.

