Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa NSosyal, Erdogan alisema kuwa baraza hilo linaunganisha jitihada za kuinua wanawake na familia.

Emine Erdogan ahimiza ushirikiano wa wanawake katika nchi za Kiturki

Mke wa rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan, ametoa wito wa ushirikiano kwa akinamama katika jumuiya ya nchi za Kiturki.

Akizungumza siku ya Ijumaa kwenye baraza maalumu la familia na wanawake jijini Ankara, Mama Erdogan alisema kuwa upekee wa nafasi ya wanawake katika jamii, umejikita kwenye utamaduni wa Kiturki.

“Tunahitaji kufanya mageuzi ya kweli, yatakayorandana na jumuiya ya Kiturki,” alisema.

Jithihada za kuwezesha familia na akinamama

“Tunalenga kuliugeuza baraza letu kama jukwaa la ushirikiano,” alieleza.

Mama Erdogan alionesha matumaini kuwa, kikao cha kwanza cha baraza hilo, kitafanyika wakati wa mkutano wa 14 wa OTS, utakaofanyika nchini Uzbekistan, mwakani.

Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa NSosyal, Erdogan alisema kuwa baraza hilo linaunganisha jitihada za kuinua wanawake na familia.

“Ni imani yetu kuwa, lolote linawezekana kwa kuwawezesha wanawake,” alisema.

Likiwa limeandaliwa na Mama Erdogan, kikao hicho kimewaleta pamoja wake za viongozi wanaohudhuria mkutano wa 13 wa OTS, familia ya Kituruki, Waziri wa Huduma za Jamii Mahinur Ozdemir Goktas na wawakilishi waandamizi kutoka nchi wanachama.

TRT Afrika / AA — TRT Afrika / AA

#