DRC inadai kuendelea na mipango ya kuandaa mbio za 'Grand Prix' nchini Rwanda, Formula 1 inasaidia "kurekebisha taswira ya kiongozi wa kimabavu."
Licha ya mbio za Formula 1 kurejea barani Afrika baada ya miaka inajiandaa kurejea barani Afrika kwa mara ya kwanza katika kipindi miaka 33, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imekosoa uamuzi wa kuipa Rwanda, fursa ya kuandaa mashindano hayo makubwa ulimwenguni.
Akizungumza siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC, Therese Kayikwamba, alisema kuwa, hatua hiyo inalenga Kayikwamba alieleza kuwa, uamuzi huo unalenga “kusafisha taswira ya kiongozi mwenye uongozi wa kiimla”.
Siku ya Jumanne, Rais wa Rwanda Paul Kagame alitangaza tukio hilo akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Formula 1, Stefano Domenicali, na rais wa Shirikisho la Kimataifa la Magari (FIA), Mohammed Ben Sulayem.
Kulingana na F1, tukio hilo linatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2030 kwenye eneo maalumu huko Bugesera, karibu na mji mkuu wa Rwanda, Kigali.
Afrika Kusini, ilikuwa mwenyeji wa Formula 1, wakati mbio hizo za kimataifa zilivyofanyika barani Afrika, mwaka 1993.
DRC inaituhumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23 mashariki mwa DRC—tuhuma ambazo Rwanda imekuwa ikizikanusha mara kwa mara.
"Februari 2025, nilimuonya Stefano Domenicali na viongozi wa F1 kwamba kuruhusu Rwanda kuandaa mbio za 'Grand Prix' ni jambo lisiloweza kutetewa kimaadili," alisema Therese Kayikwamba Wagner katika taarifa yake.
"Ingawa DRC inapongeza hatua ya kuirejesha Formula 1 barani Afrika, kumpa Paul Kagame jukwaa kama hili kutasaidia kurekebisha taswira ya kiongozi wa kimabavu ambaye serikali yake imechangia kuchochea vita vya uharibifu mkubwa nchini mwetu," aliongeza.
Waziri huyo alibainisha kuwa DRC inaunga mkono ombi la Afrika Kusini la kutaka kuandaa mbio hizo, kama mbadala wa Rwanda.
"Hii pia ni fursa kwa F1 kuwaonesha watazamaji na mashabiki wake kiini halisi cha mchezo huu," aliongeza.
Alisisitiza kuwa uandaaji wa mbio hizo lazima uambatane na hatua madhubuti na huru za udhibiti, ili kuhakikisha kuwa hakuna ufadhili unaotokana na madini yanayohusishwa na migogoro au unyonyaji wa rasilimali za DRC.
Hapo awali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilipinga mipango mingine ya Rwanda inayolenga kukuza taswira yake kupitia michezo, hasa mfululizo wa mikataba mikubwa ya udhamini na klabu maarufu za soka barani Ulaya.
Mwezi Machi mwaka huu, Marekani ililiwekea vikwazo jeshi la Rwanda na maafisa wanne wa ngazi ya juu wa kijeshi, kwa madai kuwa waliunga mkono waasi wa M23 Mashariki mwa DRC.
Rwanda ilipinga vikwazo hivyo, ikiviona kuwa vya upendeleo na kusema kuwa vinatoa taswira isiyo sahihi kuhusu mzozo huo.

