Dollar

38,5924

0.02 %

Euro

43,8834

0.36 %

Gram Gold

4.231,9700

2.37 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) linatarajiwa kufanya mjadala wa dharura tarehe 7 Mei 2025 kujadili hali ya kisiasa nchini Tanzania.

Bunge la Ulaya kujadili swala la Lissu

Mjadala huo, unatarajiwa kujikita zaidi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu, na athari zinazoweza kutokea katika demokrasia ya nchi hiyo iwapo Lissu atapatikana na hatia ya uhaini.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye tovuti ya Bunge hilo, mjadala huo utafanyika kati ya saa 7 mchana hadi saa 4 usiku kwa saa za Ulaya ya Kati (CET). 

Baada ya mjadala huo, Wabunge hao watalijadili na kulipigia kura  azimio hilo siku ya pili ambayo itakuwa tarehe 8 Mei 2025.

Azimio hilo litaangazia moja kwa moja kesi ya Lissu pamoja na maendeleo ya hivi karibuni ya kisiasa nchini Tanzania. Hayo yakijiri, kesi mbili zinazomkabili Tundu Lissu zikiendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Lissu anakabiliwa na mashtaka mawili tofauti ya jinai: kesi ya uhaini na kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii.Hata hivyo, kesi ya uhaini haina dhamana. 

Lissu alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashtaka hayo tarehe 10 Aprili 2025.

Bunge la Ulaya limekuwa likifuatilia kwa karibu masuala ya haki za binadamu na demokrasia nchini Tanzania, na mjadala huu unatarajiwa kuwa hatua muhimu katika kuangazia changamoto za kisiasa na hali ya haki za kiraia nchini humo.

Hata hivyo, baadhi wameanza kulalamikia hatua hiyo, na kusema, Tanzania ni nchi huru, hivyo haitakiwi kuingiliwa katika mambo yake ya ndani.Ikumbukwe kuwa, haya yanajiri wakati taifa hilo la Afrika Mashariki linajiandaa kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#