Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Askofu Ruwa'ichi ametoa kauli hiyo wakati wa homilia yake ya Novemba 10, 2025 katika Ibada ya Misa ya kuwaombea waliofariki wakati wa vurugu baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, nchini Tanzania.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaues Ruwa'ichi amesema kuwa mauaji ya waandamanaji yanabaki kuwa chukizo mbele za Mungu.
Askofu Ruwa'ichi ametoa kauli hiyo wakati wa homilia yake ya Novemba 10, 2025 katika Ibada ya Misa ya kuwaombea waliofariki wakati wa vurugu baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, nchini Tanzania.
"Taifa letu limejeruhiwa na Taifa letu limepoteza heshima kutokana na yale yaliyojiri wiki ya uchaguzi mkuu," amesema Askofu Mkuu Jude Thaddaeus katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jijini Dar es Salaam.
Kulingana na kiongozi huyo wa dini, sio tu limepoteza heshima, taifa hilo pia limepoteza watu, ambao waliuwawa kiholela.
Alisema: Kuna watu waliuwawa wakiandamana lakini adhabu ya kuandamana sio kifo cha risasi.
“Matendo kama haya, ni chukizo mbele za Mungu.”
Comments
No comments Yet
Comment