Serikali ya Afrika Kusini yakiri matumizi yasiyodhibitiwa ya AI yamechangia kosa kwenye sera ya taifa.
Waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini, Solly Malatsi, amesema tukio la kuwepo kwa marejeo ya uongo kwenye rasimu ya sera ya taifa ya AI linaonyesha umuhimu wa usimamizi makini wa binadamu katika matumizi ya teknolojia ya akili bandia.
Akizungumza baada ya serikali kuondoa rasimu hiyo, Malatsi alisema matumizi ya AI bila uhakiki wa kutosha yanaweza kuhatarisha uaminifu wa nyaraka muhimu za kitaifa.
Alisema serikali imepokea tukio hilo kama funzo kubwa kuhusu hatari za kutegemea AI bila udhibiti wa kibinadamu.
Waziri huyo aliongeza kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya waliohusika katika kuandaa waraka huo wenye dosari.