Tofauti zajitokeza kati ya tathmini ya Pentagon na kauli za Donald Trump.
Wabunge nchini Marekani wameonyesha kutoridhishwa na tathmini ya Pentagon kuwa uondoaji wa mabomu katika Mlango Bahari wa Hormuz unaweza kuchukua hadi miezi sita.
Ripoti hiyo inakinzana na kauli ya Rais Donald Trump aliyedai kuwa mabomu hayo tayari yanaondolewa au yameondolewa kwa msaada wa Marekani.
Wakati huo huo, Iran imekanusha madai ya kuweka mabomu hayo, huku Majid Takht-Ravanchi akisisitiza kuwa tuhuma hizo hazina msingi.
Tofauti hizi zimeongeza sintofahamu kuhusu hali halisi ya usalama katika njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.
CHANZO: Newstimehub