Urusi imedai kuwa picha za video zinaonyesha mapambano dhidi ya waasi wa Tuareg, huku uhalisia wake ukitiliwa shaka,
Madai mapya kutoka Russia yamezua mjadala baada ya kusambaa kwa video inayodaiwa kuonyesha mapigano dhidi ya waasi wa Tuareg nchini Mali,kwa mujibu wa mamlaka za Urusi, video hiyo inaonyesha vikosi vinavyoshirikiana nayo vikikabiliana na wapiganaji wa Tuareg katika maeneo yenye migogoro kaskazini mwa Mali, Hata hivyo, hakuna uthibitisho huru uliothibitisha uhalisia wa video hiyo.
Wataalamu wa usalama wanasema kuwa katika migogoro ya kisasa, video na taarifa kama hizi mara nyingi hutumika kama zana ya propaganda ili kuonyesha nguvu au kudhoofısha upande wa pili.wa upande wa Mali, serikali inaendelea kupambana na makundi mbalimbali yenye silaha, yakiwemo yale yanayotaka kujitenga au kupata mamlaka zaidi katika maeneo yao.
Hali hiyo imeifanya kanda ya Sahel kuwa moja ya maeneo yenye changamoto kubwa za kiusalama duniani, huku juhudi za kimataifa zikiendelea kutafuta suluhisho la kudumu.
Chanzo:Newstimeshub