Baada ya mashambulizi kusababisha vifo vya watu 10, Ukraine imechukua hatua ya kulenga miundombinu ya mafuta ya Urusi.

Ukraine Yajibu Mashambulizi ya Urusi Kwa Kulenga Sekta ya Nishati.

Mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na Russia yamesababisha vifo vya watu 10 nchini Ukraine, huku wengine wengi wakijeruhiwa na kupoteza makazi yao.

Taarifa zinaeleza kuwa mashambulizi hayo yalikuwa makali na yalilenga maeneo yenye watu wengi pamoja na miundombinu muhimu kama umeme na barabara, hali iliyosababisha usumbufu mkubwa wa maisha ya kila siku kwa wananchi.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alisema kuwa nchi yake haiwezi kukaa kimya wakati raia wake wanashambuliwa, hivyo imeamua kuchukua hatua za kujilinda na kujibu mashambulizi hayo.

Alieleza kuwa Ukraine imelenga meli za mafuta na vituo vya kuhifadhi mafuta vinavyotumiwa na Urusi, akisisitiza kuwa sekta ya nishati ni mhimili muhimu katika kuendesha shughuli za kijeshi.

Wachambuzi wanasema kuwa kulenga miundombinu ya mafuta kunaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Urusi na uwezo wake wa kuendeleza vita, lakini pia kunaweza kusababisha athari kwa soko la mafuta duniani,

Hali ya usalama katika eneo hilo inaendelea kuwa tete, huku mashambulizi ya mara kwa mara yakiripotiwa na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi

Chanzo:Newstimeshub .

#