Dollar

42,5810

0.01 %

Euro

49,6455

0.07 %

Gram Gold

5.716,7200

-0.35 %

Quarter Gold

9.509,9300

0 %

Silver

79,2600

-0.38 %

Mara kwa mara, chama cha upinzani cha Bobi Wine kijulikanacho kama National Unity Platform, kimeituhumu serikali ya Museveni kwa kuhusika na utekaji na utesaji wa wanachama wake.

Uganda: Jeshi la Polisi kuchunguza madai ya askari wake kuwachapa fimbo wapinzani

Jeshi la Polisi nchini Uganda limesema kuwa litafanya uchunguzi kuhusu madai ya maofisa wake kuwashambulia kwa fimbo baadhi ya wafuasi wa upinzani, akiwemo mgombea urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine.

Kupitia ukurasa wake wa X, Bobi Wine alidai kushambuliwa na mmoja wa ulinda usalama kwa kupigwa na fimbo usoni, wakati wa kampeni zake zilizofanyika Kaskazini mwa Gulu.

"Tumepokea taarifa za baadhi ya maofisa kuwachapa bakora raia. Tunajutia vitendo hivi," lilisema jeshi hilo kupitia tovuti yake.

Wine, mwenye umri wa miaka 81, atakabiliana na Rais Yoweri Museveni katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Januari 15, 2025.

"Matukio yoyote ambayo yataonekana kwenda kinyume na taratibu tulizokubaliana, zitachunguzwa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya askari yoyote atakayepatikana na kosa,” liliongeza jeshi hilo.

Mara kwa mara, chama cha Wine kijulikanacho kama National Unity Platform, kimeituhumu serikali ya Museveni kwa kuhusika na utekaji na utesaji wa wanachama wake.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#