Simba imeibuka bingwa wa Kombe la Muungano baada ya ushindi mwembamba dhidi ya Yanga.
Katika dabi kali iliyovuta hisia za mashabiki, Simba SC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano baada ya kuifunga Young Africans SC bao 1-0.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Amaan Complex ilikuwa na ushindani mkali sana, huku kila timu ikipata nafasi kadhaa za kufunga lakini kukosa umakini katika umaliziaji.baada ya sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90, mchezo uliingia katika muda wa nyongeza, Hapo ndipo Selemani Mwalimu alipoibuka shujaa kwa kufunga bao muhimu lililowapa Simba ushindi na ubingwa.
Kocha wa Simba alisifu juhudi za wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika za mwisho, huku upande wa Yanga ukiahidi kurejea kwa nguvu katika mechi ijayo ya ligi, mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu mechi nyingine kati ya timu hizi mbili tarehe 3 katika NBC Premier League, ambayo inatarajiwa kuwa na presha kubwa zaidi.
Chanzo:Newstimeshub
