Hakuna mshindi aliyepatikana kati ya Atletico Madrid na Arsenal katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Champions League.

Sare ya 1-1 Yaiweka Nusu Fainali Kati ya Atletico na Arsenal Wazi.

Atletico Madrid na Arsenal zimepambana vikali na kumaliza kwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League,Arsenal walionyesha nidhamu kubwa katika kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao kupitia penalti, huku wakidhibiti mchezo kwa kiasi kikubwa kabla ya mapumziko. 

Baada ya mapumziko, Atletico walibadilika kabisa na kuanza kushambulia kwa nguvu zaidi, jambo lililowasaidia kupata penalti na kusawazisha mchezo,mchezo huo pia ulikuwa na matukio ya utata, hasa kuhusu maamuzi ya VAR, ambapo penalti ya Arsenal ilifutwa licha ya wachezaji kudai kulikuwa na madhambi ya wazi.

Sasa timu zote mbili zinajiandaa kwa mechi ya marudiano, ambapo mshindi ataenda fainali ya mashindano hayo makubwa barani Ulaya.

Chanzo:Newstimeshub 

#