Dollar

40,4343

0.24 %

Euro

47,1614

0.49 %

Gram Gold

4.349,9900

0.54 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

''Sote inabidi tuunge mkono mwendelezo wa maendeleo hadi tamati,'' inasema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda

Rwanda yapongeza makubaliano ya DRC ya kusitisha mapigano na waasi wa M23 kama 'hatua muhimu'

Rwanda imepongeza kutiwa saini mjini Doha kwa tamko la kanuni kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na muungano wa makundi mbalimbali ya waasi yanayojumuisha M23 (AFC/M23), kama hatua muhimu ya kuelekea katika utatuzi wa amani wa mzozo wa mashariki mwa Congo.

Tamko hilo la kanuni lilitiwa saini Jumamosi na wawakilishi kutoka pande zote mbili, kufuatia wiki za mazungumzo ya kidiplomasia.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imesema makubaliano hayo yanaunga mkono njia ya mapatano ya amani yaliyowezeshwa na Qatar.

"Tamko la leo huko Doha ni hatua muhimu kuelekea utatuzi wa amani wa mzozo wa mashariki mwa DRC, kwa kushughulikia sababu kuu za mzozo na kurejesha usalama na utulivu katika eneo letu," ilisema taarifa hiyo mwishoni mwa Jumamosi.

‘Amani ya kudumu’

Rwanda ilipongeza jukumu la upatanishi la Qatar pamoja na uungaji mkono wa Marekani, ambao ilisema unatokana na juhudi za Umoja wa Afrika pamoja na mipango mingine ya kambi za kikanda.

"Sote tunapaswa kuunga mkono mwendelezo wa maendeleo hadi mwisho. Rwanda inasalia kujitolea kuchangia amani endelevu pamoja na maendeleo ya kiuchumi katika eneo la Maziwa Makuu," ilisema.

Makubaliano hayo yamekuja wiki kadhaa baada ya Rwanda kutia saini makubaliano ya amani na DRC Juni 27, mjini Washington, ambayo yanaibua matumaini ya kumaliza mapigano makali mashariki mwa Congo.

DRC na mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 tangu kuibuka tena mwaka 2021, madai ambayo Rwanda inakanusha mara kwa mara.

Kundi la waasi lililo katikati mwa mzozo wa mashariki mwa Congo linadhibiti maeneo makubwa, ikiwa ni pamoja na miji mikuu ya majimbo ya Goma na Bukavu iliyotekwa mapema mwaka huu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#