Mamlaka za Madagascar zinamshikilia raia wa Ufaransa zikidai alihusika katika mipango ya kuvuruga utulivu wa nchi.

Raia wa Ufaransa Ashikiliwa Madagascar Kwa Tuhuma za Njama za Kisiasa

Serikali ya Madagascar imemshikilia raia wa France anayeshukiwa kushiriki katika njama za kisiasa zinazolenga kuleta machafuko nchini humo,Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, mtuhumiwa anadaiwa kuhusika katika kupanga mikakati ya kuhamasisha maandamano yasiyo rasmi pamoja na kueneza taarifa zinazoweza kuchochea hasira za wananchi dhidi ya serikali. Inaelezwa kuwa shughuli hizo zilikuwa zinafanyika kwa siri na zilikuwa zikilenga kuathiri utulivu wa kijamii.

Mamlaka za usalama zimebainisha kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini iwapo kuna mtandao mpana zaidi unaohusisha watu wengine wa ndani na wa nje, Serikali imeahidi kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika vitendo hivyo.

Tukio hilo meibua mjadala mkubwa ndani ya nchi, ambapo baadhi ya wananchi wanaunga mkono hatua ya serikali kama njia ya kulinda usalama wa taifa, huku wengine wakitaka uwazi zaidi katika mchakato wa uchunguzi.Kwa upande wa kimataifa, tukio hili linafuatiliwa kwa karibu France, ambayo imeeleza umuhimu wa kuhakikisha haki na taratibu za kisheria zinafuatwa kikamilifu.

Wataalamu wa masuala ya usalama wanasema kuwa matukio kama haya yanaonyesha changamoto ya kudhibiti ushawishi wa nje katika siasa za nchi zinazoendelea.

Chanzo:Newstimeshub 

#