Afisa huyo wa zamani asema kushindwa kudhibiti walowezi wenye silaha kunaweza kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Baada ya kulaani mashambulio ya walowezi dhidi ya Wapalestina, Tamir Pardo ameonya kuwa hali hiyo inaweza kuisukuma Israel kwenye mgogoro mkubwa wa ndani.
Kwa mujibu wa Pardo, baadhi ya walowezi wenye msimamo mkali wana silaha na wanaungwa mkono kisiasa na viongozi wa mrengo wa kulia ndani ya serikali ya Israel.
Amesema jaribio lolote la kuwadhibiti kwa nguvu linaweza kusababisha mivutano mikubwa ya ndani na hata kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Aidha, alilaumu vyombo vya sheria vya Israel kwa kufahamu kinachoendelea lakini kushindwa kuchukua hatua madhubuti.
CHANZO: Newstimehub