Trump: Iran imewasiliana moja kwa moja na Marekani, inataka kufikia makubaliano
Rais Trump amesema Iran imewasiliana moja kwa moja na Marekani ikitaka kufanya mazungumzo ya kufikia makubaliano, huku Marekani na Iran zikiendelea kutofautiana kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz.
17 Septemba 2026
Pakistan yalaani “jaribio la shambulio la droni” karibu na Makkah
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, ameunga mkono Saudi Arabia baada ya mifumo yake ya ulinzi wa anga kuizuia droni karibu na mji mtakatifu wa Makkah, huku akitoa wito wa kujizuia kutokana na kuongezeka kwa mvutano
16 Septemba 2026
Kim Jong Un atangaza kumuunga mkono Putin
Ushirikiano kati ya mataifa hayo, umeendelea kuongezeka tangu mataifa hayo yalipokubaliana kushirikiana, mwezi Juni 2024.
15 Septemba 2026
Iran yaweka mpango wa dharura kukabiliana na vita, usitishaji mapigano na kipindi cha baada ya vita
Maelekezo hayo yanataka hatua tofauti zichukuliwe na umma pamoja na taasisi, kutegemea iwapo mapigano yataendelea, yatasitishwa kwa muda au yatafikia mwisho.
15 Septemba 2026
Kaka mkubwa wa mfame mpya wa Tooro, afariki
Inaripotiwa kuwa mwana wa mfalme huyo alikuwa akipambana na saratani kwa zaidi ya mwaka mmoja.
15 Septemba 2026
Iran, UAE zakubaliana kuboresha uhusiano na kuimarisha ushirikiano: Pezeshkian
Rais wa Iran amesema mazungumzo yake na Mwanamfalme wa Abu Dhabi yalilenga mustakabali wa uhusiano kati ya nchi hizo pamoja na maendeleo ya kikanda.
14 Septemba 2026
Tangazo · 970 × 250
Mfalme Oyo Nyimba kuzikwa leo kwa mujibu wa mila na desturi
Viongozi wa ukoo wa kifalme wamemchagua binamu yake Oyo, Edward Rukidi Kijanangoma, kuwa mfalme mpya.
12 Septemba 2026
Korea Kusini: Hatujaamua bado kuhusu kutuma vikosi katika Mlango-Bahari wa Hormuz
Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Cho Hyun, amemweleza mwenzake wa Iran kwamba Korea Kusini inaunga mkono hatua za kuhakikisha meli zinaweza tena kupita kwa usalama katika njia hiyo muhimu ya kimkakati.
11 Septemba 2026
Mahakama yakataa ombi la Lissu kumuita Rais Samia kutoa ushahidi
Mahakama imekubali ombi la upande wa Utetezi la kuwaita viongozi watatu wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushahidi.
10 Septemba 2026
Trump awaahidi raia wa Marekani $5,000 kila mmoja iwapo Republican watashinda uchaguzi
Rais hakusema fedha hizo zitatoka wapi -- huku gharama zikitarajiwa kuwa zaidi ya $1 trilioni.
10 Septemba 2026
Ndege ya Rais Zelenskyy karibu kugongwa na droni: Waziri Mkuu wa Norway
Rais wa Ukraine, Zelenskyy, aliwasili Oslo akitokea Moldova jioni ya Jumanne kuhudhuria mazishi ya Mfalme Harald V wa Norway.
9 Septemba 2026
Israel yaagiza kufungwa kwa ubalozi wa Uingereza Jerusalem Mashariki inayokaliwa ndani ya siku 30
Israel imeitaka Uingereza kufunga ubalozi wake mdogo katika Jerusalem Mashariki inayokaliwa na kuwafukuza maafisa wa ubalozi wakilipiza hatua ya Uingereza kuwawekea vikwazo walowezi wa Kiisrael katika Ukingo wa Magharibi
9 Septemba 2026
Putin amuambia Trump: Urusi haina nia ya kuzishambulia nchi za Ulaya
Rais wa Marekani na mwenzake wa Urusi wamejadili juhudi za amani kufuatia ziara za wajumbe wa Marekani jijini Moscow na Kiev.
8 Septemba 2026
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yatoa wito wa kulindwa kwa Wapalestina, yapinga kuondolewa kwa lazima
Mawaziri wa mambo ya nje wametoa wito wa utekelezaji kamili wa usitishwaji mapigano Gaza, kuunga mkono mpango wa ujenzi upya na kongamano la kimataifa jijini Cairo
8 Septemba 2026
Iran yaonya Korea Kusini dhidi ya kutuma vikosi vya kijeshi katika Mlango-Bahari wa Hormuz
Iran imesema ushiriki wowote wa kijeshi wa Korea Kusini katika juhudi za kuhakikisha usalama wa usafiri wa meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz utakuwa na madhara makubwa.
7 Septemba 2026
Qatar: Nchi za Ghuba haziwezi kutegemea Marekani pekee kulinda usalama wao
Qatar inasema ushirikiano na Marekani unasalia kuwa muhimu, lakini hauwezi kuwa ndiyo dhamana pekee ya usalama wa kikanda katikati ya mivutano na Iran.
7 Septemba 2026
Futeni madeni yao, watumeni kuivamia Iran: Gazeti la Israel lapendekeza mpango kwa Wamarekani
Kitengo cha maoni katika gazeti la Jerusalem Post kinaelezea jinsi serikali ya Marekani inaweza kutumia madeni ya mamilioni ya Wamarekani vijana, ikitumia msamaha wa mikopo kama njia ya kuwasukuma kupigana Iran.
5 Septemba 2026
Urusi, Ukraine washambuliana kwa droni huku makao makuu ya usalama Ukraine yakilengwa
Mashambulizi ya droni ya Urusi yamejeruhi watu watano katikati mwa mji wa Kiev huku mashambulizi ya Ukraine yakisababisha moto katika kituo cha mafuta karibu na mji wa Sochi, kuonesha hatari ya vita hivyo huku pande zote
4 Septemba 2026
Raia wa Marekani waokolewa baada ya mashambulizi katika kambi ya mbuga ya wanyamapori Msumbiji
Msumbiji imekuwa ikikabiliana na ugaidi katika mkoa wa kaskazini wenye utajiri wa gesi wa Cabo Delgado tangu 2017, mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu na maelfu wengine kuondoka kwenye makazi yao.
4 Septemba 2026
Trump: Marekani inapigana na Iran kulinda washirika wake Mashariki ya Kati na Magharibi
Trump pia amedai kuwa Iran inaweza kuwa tishio kwa Ulaya na baadhi ya miji ya Marekani katika siku zijazo.
3 Septemba 2026
Netanyahu awashutumu wakuu wa usalama kwa kukosa makusudi kumwamsha mnamo Oktoba 7
Madai yanajitokeza huku Netanyahu akikabiliwa na ukosoaji endelevu kuhusu dhima yake katika mapungufu ya kiusalama yaliyohusiana na shambulio la ghafla la tarehe 7 Oktoba.
2 Septemba 2026
Iran yawataka raia wake kupunguza matumizi ya petroli
Wiki iliyopita, Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Jafar Ghaempanah, alikaririwa akisema kuwa, uzalishaji wa ndani wa petroli haukuwa wa kuridhisha.
1 Septemba 2026
Marekani yashambulia Kisiwa cha Iran, kadhaa wauawa na kujeruhiwa
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) kimesema shambulio la Marekani limewaua na kuwajeruhi wanachama kadhaa wa IRGC pamoja na raia, huku wakiahidi kulipiza kisasi na kutoa “adhabu kwa mchokozi”.
31 Agosti 2026
Mbu aliyeletwa na ndege Ujerumani asababisha vifo vya watu wawili
Mamlaka ya afya ya jiji la Frankfurt ilithibitisha vifo hivyo Jumatano.
28 Agosti 2026