Serikali ya Uturuki yaanzisha uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tukio.
Kufuatia shambulizi la kutisha lililotokea mkoani Kahramanmaras, mamlaka za Uturuki zimeanza uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tukio hilo, ambalo sasa linadaiwa kuhusishwa na mwanafunzi wa darasa la nane.
Kwa mujibu wa Gavana Mukerrem Unluer, mshukiwa aliingia shuleni akiwa na silaha kadhaa zilizokuwa zimefichwa kwenye begi, na kufyatua risasi kiholela ndani ya madarasa mawili.
Rais Recep Tayyip Erdogan amesema waendesha mashtaka na mamlaka husika wanafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha ukweli wote unajulikana na hatua stahiki zinachukuliwa.
CHANZO: Newstimehub