Zaidi ya tani 200 za nyama zimekwama kwenye maghala.

Mgogoro wa Mashariki ya Kati Wapunguza Mauzo ya Nyama Kenya

Biashara ya nyama nchini Kenya imeathirika baada ya zaidi ya tani 200 za bidhaa hiyo kubaki kwenye maghala kufuatia kusitishwa kwa baadhi ya njia za usafirishaji kuelekea masoko ya Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa Meneja Uzalishaji wa Juja International Abattoirs, hali hiyo imesababishwa na kuvurugika kwa usafiri wa baharini na angani, jambo lililopunguza mauzo katika nchi kama Falme za Kiarabu na Saudi Arabia miongoni mwa zingine.

CHANZO: Newstimehub

#