Dollar

42,3422

0.16 %

Euro

49,3645

0.11 %

Gram Gold

5.718,7300

1.1 %

Quarter Gold

9.714,9300

0 %

Silver

72,5600

2.07 %

Mawaziri wa mambo ya nje wa matafia ya G7 Jumatano wamelaani vikali mashambulizi wanayoyaita “ya kikabila” yanayotekelezwa na wapiganaji wa RSF dhidi ya raia na wafanyakazi wanaotoa misaada katika miji ya El-Fasher na Kordofan Kaskazini.

Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano

“Tunalaani vitendo vya ukatili wa kingono. Tunazitaka RSF na Jeshi la Sudan (SAF) kuheshimu haki za binadamu, kupunguza mapigano, kukubaliana juu ya usitishaji wa mapigano wa haraka na wa kudumu, na kuruhusu misaada ya kibinadamu kufika kwa haraka na bila vizuizi,” ilisema taarifa hiyo.

Mawaziri hao pia walionyesha uungwaji mkono wao kwa “jitihada za kidiplomasia zinazoendelea kurejesha amani na usalama,” na wakazitaka nchi nyingine kushiriki katika juhudi hizo.

Haya yanajiri baada ya Umoja wa Mataifa ukionya kuwa hali nchini Sudan inazidi kuwa mbaya kwa raia, huku mashirika ya misaada yakionyesha kuwa ufikiaji wa maeneo yaliyoathiriwa bado unazuiliwa na vita.

Mzozo wa umwagaji damu kati ya jeshi na RSF, ambao ulianza Aprili 2023, umeua watu wasiopungua 40,000 na wengine milioni 12 kuyahama makazi yao, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni.

Mwezi uliopita, RSF iliteka mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, El-Fasher, na kutuhumiwa kwa mauaji.

Kundi hilo linadhibiti majimbo yote matano ya Darfur kati ya majimbo 18 ya Sudan, wakati jeshi linashikilia majimbo 13 yaliyosalia, pamoja na Khartoum.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#