Malalamiko yaongezeka huku mashirika yakishutumu FIFA kwa bei zisizo na uwazi.
Mashabiki na mashirika ya watumiaji barani Ulaya wamepinga vikali bei za juu za tiketi za Kombe la Dunia 2026, wakidai FIFA inatumia nafasi yake vibaya na kuweka mfumo usio na uwazi wa ununuzi wa tiketi.
Wachambuzi wanasema bei za tiketi zimepanda kutokana na mfumo wa “dynamic pricing” unaobadilika kulingana na mahitaji ya soko, hali inayowafanya mashabiki wengi kushindwa kumudu gharama za mashindano hayo makubwa.
FIFA hata hivyo imeendelea kusisitiza kuwa mfumo huo unaendana na mahitaji makubwa ya mashabiki duniani.
CHANZO: Newstimehub